Jumatano, 21 Juni 2017

MAJONZI MAKUBWA KATIKATI YA FURAHA

Tags


Baada ya jamaa kutangaza uchumba na dada mmoja, kumbe dada mtu anamfahamu vizuri sana huyu mchumba wa kaka yake ambaye ni wifi yake na wamesoma wote secondary kidato cha kwanza mpaka cha nne lakini walipotezana miaka mingi.

Ilikuwa ni ijumaa moja ambapo jamaa aliamua kumpeleka kwa wazazi wake,na alikwisha waandaa wiki moja nyuma, kwa hiyo walikuwa wamejiandaa akiwepo na wifi japo mpaka hapo hakujua ni MTU wa aina gani anaekuja kutambulishwa.

Ilikuwa majira ya saa 7 jamaa na mchumba wakawa wameshatia timu nyumbani kwa baba na nama.

Walipoingia tu ndani ya geti dada mtu akachungulia kupitia dirishani amwone wifi yake,akashangaa kumwona Beatrice waliesoma wote. gafla akawa amekasirika vibaya mno akikumbuka historia ya mwenzie huyo haikuwa ni nzuri miaka hiyo ya nyuma.

Walipoingia ndani sebuleni familia nzima wakamkaribisha kwa furaha mgeni kasoro veronica alikuwa amekosekana sebuleni akawa amejifungia ndani.....

alipogongewa akatoa udhuru kana kwamba tumbo limechafuka ghafula lakini angetoka baada ya dakika chache,lakini kusema ukweli alikuwa amelala anachati na marafiki zake kupitia group la whatsap la wanafunzi wenzake waliomaliza pamoja akimkejeri kaka yake kwa uamuzi wa kuoa mtu ambaye alishawahi kubakwa na wanaume zaidi ya 6

basi wenzie walianza kutuma katuni๐Ÿ˜‚๐Ÿ’‡๐Ÿ˜ท za kuonyesha kumlilia kumsikitikia huyo brother.....

"Heheheeeee ngoja niende sebuleni nikamwone wifi jamen!!!aliwaaga wenzie group wengine wakamjibu " atashtukajee!!!

ataona aibu huyoo! Anataka kumwuua kaka wa sie!!tena hawezi kukosa kuwa na magonjwa huyo. Alijibu mmoja wa marafiki zake.vero akazima data.

Basi walipokuwa wapo karibu na kumaliza vero akatoka akiwa amenuna akafika sebuleni.

He!wewe ni veroo! Waoo rafkiang!!

alisema kwa furaha Beatrice akisimama kwenda kumuwao vero,lakini vero alikuwa kawaida tu akamsalimia na kukaa........kile kitendo kilimuudhi kaka yake akamuuliza mchumba wake,

"Unamjua vero?

Yes tumesoma wote alipokea Beatrice.

Akapokea baba " wewe vero kumbe unamfahamu WiFi yako mbona huonyeshi kufurahi?

Hapana baba mbona nimefura tu!!karibu sana wifi tunakupenda alijibu vero

"Asante sana mwe nimefrahi kumbe wewe ni WiFi kweli Mungu ana makusudi, tulikuwa marafiki shuleni lakini sasa ni zaidi ya rafiki hakika Mungu ni Mkuu! Alisema Beatrice kwa Furaha.....vero hakuwa mwenye Furaha kusema ule ukweli.

Basi walipomaliza ,wakataka kutawanyika,Beatrice akasema akaomba kusema kidogo.

"samahani sana baba na mama na WiFi yangu na shemeji zangu kwa kunikaribisha ,sina mengi ya kusema na samahani kwa Uhuru wangu wa kuwa msemaji wakati sio vizuri sana kuwa msemaji sana kwa wakwe zako ,nafikiri nimeshindwa kuzuia Furaha yangu hasa nilipomuona vero,tulipotezana kama miaka 6 hivi hata kimawasiliano........kuna vitu vingi vibaya tulivifanya wakati huo kwa sababu ya ujana ulikuwa ni mwingi....

Akamgeukia vero na kumwambia "kwasasa sio yule wa miaka ile
Nimeokoka nampenda Mungu......amenifanya kiumbe kipya......
Beatrice akaanza kutokwa na machozi sijui alikumbuka nini.
Nafkir alikuwa anajua fika kwamba vero atavuruga uhusiano wao kutokana na hali aliyoiona pale sebuleni.

Basi mchumba wake akamkumbatia akawa anampiga kifuani akaanza kulia nae,wazazi hawakuwa wanaelewa kinachoendelea
Vero anajua kinachoendelea
Beatrice anajua kinachoendelea

John anajua kinachoendelea,maana historia yote mchumba wake alishamwambia mapema,vile alivyowahi kubakwa alipokuwa na rafiki zake moja ya fukwe za bahari.

 week end moja walienda beach wenzie wakaingia baharini kuogelea lakini yeye alikuwa anaogopa,baadae kuna vijana wakamshawishi kuingia kwenye tube moja la kuogelea wakimwambia hawatampeleka mbali,basi alipoingia tu,wakampeleka kwenye kina kirefu ambako walimfanyia upuzi wote huko hasa wakitumia vidole......alijaribu kupiga kelele lakini kwenye maji sauti haifiki mbali.......

Wenzie walipotoka nje kama saa 11 jioni akiwemo na vero walipomkosa hawakujari,walichojua ameamua kuondoka lakini kumbe mwenzao yuko majini wakawa wameondoka eneo hilo.

Beatrice Kule majini akawa hali mbaya kalipoingia kagizagiza wakaamua wamtoe nje na kumbaka kwa kupokezana na akawa amepoteza ufahamu, wakamwacha ,baadae wasamalia wema wakaita police wakamkimbiza hospital na akawa ameshonwa kutokana na kumchana sehemu za siri na waandishi wa habari wakamchukua Picha na kesho yake ikatoka habari ile na picha zikachukuliwa.

Taarifa zikawafikia ndugu wakafika hospital Beatrice alipopata fahamu police wakachukua maelezo yake wakagundua kuwa mara ya mwisho alikuwa na wenzie [wakina veronica] wakaenda kuchukuliwa na kuwekwa ndani lakini baadae walikuja kuachiwa kwa dhamana,ni story ndefu mimi naenda kwa kifupi.......

Beatrice akiwa amekumbatiwa na mchumba wake wakilia,baba akawauliza KWANINI MAJONZI MAZITO KATIKATI YA FURAHA?

John akasema"nakupenda kuliko chochote dear wewe unamcha Mungu,biblia inasema  usiyatafakari mambo yaliyopita maana Mungu ni wa mambo mapya siku zote......

niko tayari kulia na wewe na kufurahi na wewe siku zote....

akachukua kitambaa na kumfuta mchumba wake.

"Asante my alijibu Beatrice.
Akachukua hicho kitambaa akamfuta john
Thanks, alijibu john.

Baada ya hapo Beatrice mwenyewe akasema naomba nimshukuru Mungu kwa siku kubwa kama hii,wote wakafunika macho.

"Mwenyezi Mungu Baba wa rehema
Asante kwa kutukusanya leo na familia hii,
Nakushukuru kwa kunipenda na kunithamini
Umenistahilisha wakati nilikuwa sistahili
Laiti kama ungelihesabu makosa yetu tusingekuwa na ujasiri wowote wa kusimama mbele zako wala kuomba chochote......tunapotoka mahali hapa,ulinzi wako uwe nasi amen!wote wakaitikia amen!

Wakakumbatiana lakini wakati akiwa anaomba vero alikuwa ameshatoka na kuingia chumbani kuchati na marafiki zake kuwapa feedbacks....

Wanapoagana Beatrice akasema naomba mniagie WiFi yangu mama,mama akajibu "naona ako na mchafuko wa tumbo kidogo aliongea ili kumtetea tu.

Baba na mama na watoto waliporudi ndani ,wakamwita vero sebuleni wakitaka kujua nini anachojua kuhusu WiFi yake.

Siwezi,siwezi,nasema tena siwezi narudia tena kusema siwezi kumuunga mkono john kumwoa yule msichana ,eti anajifanya mlokole,mnafki mkubwa tu yule malaya,akaeleza mambo chungu nzima kumhusu Beatrice.......oneni wenyewe hii simu muone hata marafiki zangu wanavyomjua ana history chafu.....

Mdogo wake mmoja akachukua ile simu aone chatting za group

Mbona hizi chatting zole ni za nyuma lakini unajuaje labda kabadirika? Alisema huyo dogo.

Kabadirika wapi!?hakuna mwanamke palee!!alijibu vero

Baba akachukua aone nae
Ha!kumbe huyu ndiye yule binti ambaye alibakwa kipindi kile wewe nakuhangaikia police? Ndiyo baba nakumbuka ulitoa hela nyingi sana ili Mimi nitoke halafu eti ndiyo aolewe tena na kaka!?
Ametoa mimba nyingi sana Beatrice Mimi namjua ndio maana aliponiona alishtuka na kuanza kulia

Baba akamuuliza vero" kwani Beatrice alipenda kubakwa?

Huoni kama ninyi pia mlichangia kubakwa kwake?

Hii ilikuwa ni ngumu sana kwenu iwapo angekufa yule binti maana ilionekana mmeenda kumtelekeza mwenzenu kule......lakini nilienda kwa wazazi wake wakatusamehe na ilikuwa nitoe pesa za matibabu lakini wakakataa........nafurahi kwamba tunarudi tena kwao najua tunakwenda kuwapoza maumivu ya binti yao.

Vero alitaka aendelee kubisha mzee akamchapa kibao,pumbavu!,nyamaza,acha wivu na roho mbaya......vero akaamua kuondoka pale sebuleni........ Njoo hapa upesi! Mzee alimwita
"Sitaki!alijibu kwa hasira!
" sawa mwanangu mavuno yako yapo.....alijibu baba kwa upole.

"Hakuna shida,na nawaambieni akimwoa huyo msichana sintokuja kukanyaga kwake, wala harusini nisishirikishwe chochote. Alijibu tena vero.
Mama akapokea " hata usipokuja kwani Mungu anakutegemea wewe ili kufanikisha shughuli hii?Mungu ana watu wengi Mwanangu! Ila wewe unajifungia mlango maana wewe mwenyewe umeshachumbiwa tayari......sasa ukiendelea na hiyo tabia utavuruga mipango yako.......jaribu kufkir kama mchumba wako angeambiwa habar ya kiburi ulichonacho utaolewa kweli??

Kumbe mmoja wa marafiki zake alitunza kipande cha gazeti ambalo liliandika tukio la Beatrice, vero akafight mpaka akakipata na kwenda moja kwa moja kumpelekea john ili ajionee mwenyewe

Akampigia simu iwapo kama alikuwepo nyumbani, john akasema ndio karibu.......alipofika akachomoa kwenye pochi yake kipande cha gazeti na kumpa brother.......john kuangalia akakutana na kichwa cha habari chenye maandishi makubwa

BINTI ABAKWA HADI KUZIMIA UFUKWENI NA VIJANA ZAIDI YA 6 ----------------------------------++++++++++++++-------------------------------------------------\\\\\\\
Hicho kichwa cha habari kiliambatana na Picha ya Beatrice akiwa katika hali mbaya...........brother aliinama mezani na kuweka kichwa chake kwenye lile gazeti alilia sanaa kama dakika 20 huku vero akiamini sasa lengo lake limefanikiwa.......

Alipojiinua kipande cha gazeti lote kilikuwa lishalowa na machozi yake,

Aah mbona umelowanisha kabla hujasoma habari yote!!?alijibu vero huku akikichukua kile kipande,lakini john akamalizia kabisa kuchana......hivi ninavyochana ndivyo Mungu anavyozifuta history zetu chafu tunazopitia maishani ila mwanadamu hawezi kusahau.....ninachotaka kukwambia ni kwamba;

Achana na mambo ya watu wengine yasiyokusaidia chochote!

john huyu mwanamke atakuua ni mgonjwa!
Halafu ni mkubwa kwako!!alisema vero

Tumepima yuko salama hana tatizo
Hii story iliyopo kwenye gazeti alishaniambia kitambo iwapo ningekuwa tayari kuoa mwanamke wa aina yake....nilikubali.
Namimi nikamsimulia ya kwangu akasema yu tayari....miaka yake anaijua amenizidi mitatu lakini wangu sio shida,najua ana watoto wawili nje ya mimi lakini nimempenda pamoja na hao watoto wake,na ntamsaidia kuwalea.

Dada,bidii uliyotumia kutafuta hili gazeti,Kama ungeitumia kutafuta kazi ili elimu yako iwaletee matunda wazazi waliotusomesha,pengine ungekuwa kazini tayari.......

huyu vero alishachafuliwa sawa,lakini Mungu kamsafisha tayari ila wewe unataka kuanza kwa upya kumchafua tena,Mimi nakwambia humchafui yeye ila unanichafua mimi na familia yetu kwa ujumla,na huna usalama wowote kama ukiendelea na hiyo tabia dada.......Beatrice nilimpenda,nampenda,na nitaendelea kumpenda,na sintorudi nyuma kamwe! Huyu ndiye niliyepewa na Mungu.

Sijawahi kukusimulia history ya maisha yangu kwa muda ambao nimekaa mbali na wazazi wangu hata wewe hujui chochote na laiti kama ungenijua usingeendelea kumchafua Mtoto wa watu.....

Mimi nimefanya vitendo vya ujambazi vingi sana,nimemwaga damu nyingi za watu wasiokuwa na hatia lakini nimebadirika na Mungu amenisamehe japo nilijaa na lasna ya damu za watu,,,,,,nani angependa kuolewa na jambazi?

nashangaa unaniona kama malaika eti Beatrice hafai na hana sifa ya kuolewa namimi,,,,,,,,nasema hivi ,mimi ndiye nisiye na sifa ya kuwa Mume wa huyu mwanamke,lakini Mungu amenistahilisha.........

Baada ya hayo maneno ,Beatrice akawa anaingia,vero alipomwona akatoka kwa speed wakakutana mlangoni bila hata salamu

WiFi kulikoni? Beatrice alimuuliza
Vero hakujibu
Akaingia ndani akamkuta john nae ana alama za machozi mashavuni......dear umemfanya nini WiFi mbona analia
Hapana hakuna kitu dear sijui ana shida gani.....

Veronica akatoka nje akaita Bodaboda akamwambia Dereva nikimbize haraka sana usipunguze mwendo nipeleke nyumbani......

Walipokamata barabara muda wote Veronica alikuwa anajisemesha njiani......hasira zote ziliishia kwa Dereva akimfokea kwa kuendesha pikipiki taratibu......Dereva akaongeza mwendo ile anaovertake gari moja la mizigo pikipiki ikamiss akataka kutoka nje ya barabara bahati mbaya  akakumbana tax wakapigwa vibaya vero ndiye alikuwa kaumia sana akavunjika miguu yote miwili mmoja ulikatika juu ya goti mwingine ulivunjika chini kabisa sehemu kuvaa kiatu na waliseleleka na ile pikipiki ikawa imemchubua uso upande wa kushoto akawa kama ameungua.......ilikuwa ni MAJONZI makubwa lakini uzuri wake hakufa.

Ilipita miaka miwili akawa amepona ila alikuwa tayari hana Miguu ,naye alikuwa na mchumba wake akawa amemwacha kulingana na hali aliyokuwa nayo,ila kabla hajamwacha akawa amemnunulia Miguu ya bandia na ndiyo zawadi aliyomwachia.

Katika miaka miwili ambayo vero alikuwa anaugua, john na Beatrice walifanikiwa kufunga ndoa ilikuwa ni ya baraka sana haikuwa na mfano kutokana na wengi walivyomjua Beatrice wakaja kushuhudiavtukio ambalo mke na Mume wanapendana sana......

Dakika chache tu kabla john hajaenda kufunga ndoa,rafiki zake watumishi wakamwombea ili aendako aende salama......

Na tayari wana watoto wawili Enes wakike ndiye mkubwa na wapili ni wa kiume anaitwa innocent.

Nakumbuka tu maneno ya baba kwa vero
"MAVUNO YAKO YAPO MWANANGU".

Kitu cha kujifunza zaidi,kabla hamjaanza mahusiano na huyo mwenzio,muweke wazi kila kitu kihusucho maisha yako ya nyuma ,usimfiche.
Kama una watoto.
Miaka yako.
Ulishawahi kuoa au kuolewa?
mwambie ukweli maana ukimficha atakuja kujua tu,na hii ndiyo ilimsaidia Beatrice.....

KUWA MAKINI NA UNACHOPANDA SASA MAANA UTAVUNA TU HAPA HAPA DUNIANI.


By Kuhani Mlawi


EmoticonEmoticon