Ijumaa, 2 Juni 2017

KUTOKA Sioux City,Lowa,WATOTO/WADOGO ZETU WALIOPATA AJALI ARUSHA HALI ZAO ZINAVYOENDELEA

Tags

1.Mtoto Sadia na mtoto Wilson,watakuwa wanafanya"physiotherapy"(Mazoezi ya Viungo na Mwili) siku ya Jumatatu,Jumatano na Ijumaa kila wiki kuanzia sasa hadi mwisho wa mwezi June.

2.Mtoto Doreen,kuamkia leo alikuwa na "good abdominal and muscle control",yaani Mazoezi ya tumbo na Mishipa na amejitahidi kukaa mwenyewe,pia"back stitches"zimeondolewa.

3.Majadiliano yameanza kuhusu uwezekano wa kumhamisha Mtoto Doreen kutoka Mercy Hospital kwenda Kituo Maalum Cha Madonna kilichopo Omaha, Nebraska ambacho kina utaalamu wa hali ya juu Duniani kuhusu"Spine Therapy",ili Doreen apatiwe Utabibu wa hali ya juu unaowezekana kumsaidia kwenye safari yake ya kupona kutokana na upasuaji wa UTI wa mgongo aliofanyiwa. Huenda,endapo itakubalika kwa kuzingatia Ushauri wa Madaktari.
Ameandika Lazaro Nyalandu
Facebook,Tweeter



Mwangazanews
Tunawaombea kwa Mwenyezi
Mungu wapone warudi
Nyumbani.


EmoticonEmoticon