Jumapili, 11 Juni 2017

Hadithi ya 'Mrembo alalae' yageuka kuwa kweli

Tags

Hadithi ya 'Mrembo alalae' yageuka kuwa kweli:  Mtoto wa miezi sita anaejulikana kwa jina la Anya ametumbukia katika usingizi mzito wakati mama yake akimnyonyesha na kulala kwa muda wa wiki moja mfululizo katika mji wa Pervouralsk nchini Urusi.

Wazazi wake kwa walimpeleka mtoto huyo hospitalini afanyiwe uchunguzi. Mama wa mtoto huyo Aleksandr Metyolkina alisema kuwa haishi kufikiria hadithi ya mrembo alalae,ambapo mrembo huyo alilala kwa muda mrefu kabisa bila kushtuka.

Anasema ni hivyo hivyo mtoto wake Anya amelala kwa muda wa wiki moja bila kushtuka hata mara moja. Vile vile Mama huyo alisema kuwa mara ya kwanza waliogopa na kumpeleka hospitalini wakijua mtoto wao kaingia kwenye "Coma" lakini haikuwa hivyo. Daktari alisema kuwa huyo amelala fofofo.

Kwa mujibu wa habari, mtoto huyo alishtuka mara moja wakati akipelekwa hospitalini lakini aliporudi nyumbani alilala kwa mara nyingine.
Ripoti zinaonyesha kuwa mtoto huyo mara anaposhtuka tu basi uso wake huwa mwekundu,hupatwa na homa na huanza kutetemeka.

Daktari alisema "dalili hizo zinaweza kuwa zimesababishwa na moyo kwenda polepole  wakati wa mtoto huyo akiwa usingizini". Kuna wakati Madaktari walishuku inaweza kuwa ni "Meningitis" au "Encephalitis" lakini uchunguzi haukuonyesha hivyo.
Hata hivyo inasemekana kuwa joto la mtoto asiekula,asiekunywa na asiepata choo  hupungu mpaka 35.


Imeandika tovuti moja ya nchini Uturuki
Inayomirikiwa na shirika la televisheni na redio. trt.net.rt


EmoticonEmoticon