Jumanne, 30 Mei 2017

Ivan kuzikwa leo, Zari aahidi kuwaangalia watoto

Tags

Zari akiwa na watoto kwenye misa hiyo.


Baada ya Jumatatu mwili wa Ivan Ssemwanga kuangwa na kufanywa ibada takatifu,aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu,Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza.

Katika miss ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Namirembe mjini Kampala Uganda, Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.

Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhulia walijiandaa kumsikiliza atakachosema.

"Sitomhuzunikia Ivan"alisema.
"Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu tulitengana kwa sababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan.
Ivan alijua kile ninachoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua ningewaangalia vijana vyema na aliniamini.

Kwa hali hiyo,ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye."

Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili nae aliahidi kuhudhuria.

Source:bongo5.com


EmoticonEmoticon