Historia ya Kenya inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kenya.

Historia ya awali
Uvumbuzi wa majuzi karibu na Ziwa Turkana unaonyesha kwamba kiumbe kama Australopithecus anamensis aliishi katika eneo ambalo sasa ni Kenya kuanzia miaka milioni 4.1 iliyopita.
Lakini mabaki yaliyopatikana katika mabonde ya Tugen, yaliyokuwa na takriban miaka milioni 6, yalipelekea kutajwa kwa aina mpya ya spishi, Orrorin tugenensis.

Ustaarabu wa mapema Kenya
Katika milenia ya 1, wazungumzaji wa lugha za Kinilo-Sahara na lugha za Kibantu waliingia katika eneo hili, na sasa Waniloti ni 30% ya Wakenya wote. Pwani ya Kenya ikawa makao ya jamii ya wahunzi na jamii ya wakulima wadogo wadogo, wawindaji na wavuvi ambao walikuwa mhimili wa uchumi kwa kushirika katika kulimo, uvuvi, utengenezaji chuma, na kufanya biashara na nchi za kigeni.
Kuanzia karne ya 6 au karne ya 9, Kenya ilijihusisha na shughuli za ubaharia kukuza uchumi ikaanza kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.
Wafanyabiashara Waarabu walianza kwenda pwani ya Kenya mara kwa mara karne ya 1 BK. Kenya ilikuwa karibu na Peninsula ya Arabia na hii ilialika ukoloni.
Makazi ya Waarabu na Waajemi yaliongezeka kandokando ya pwani kufikia karne ya 8. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa machotara, Waafrika-Waarabu.

Mombasa ulikuwa mji wenye bandari wa nchi ya Kenya kabla ya ukoloni katika Enzi ya kati. Bandari hiyo ilitumika kuendeleza biashara na miji mingine yenye bandari Afrika, Uajemi, na wafanyabiashara Waarabu, Yemeni na hata Bara Hindi.
Baharia Mreno Duarte Barbosa wa karne ya 15 alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi, mashua nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutoka Sofala na nyingine kutoka Cambay, Melinde na nyingine zinazoabiri hadi kisiwani Unguja."
Kiswahili, ambayo ni lugha ya Kibantu iliyokopa misamiati ya Kiarabu, Kiajemi na mingine kutoka Mashariki ya Kati na Asia Kusini, baadaye ilikua ikawa lingua franca ya kibiashara kwa jamii mbalimbali.
Kwa karne nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya ni mji wa Malindi. Umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangu karne ya 14 na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwa serikali zingine.
Mwaka wa 1414, Sultani Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Uchina wa Ming, wakati wa safari za mchunguziZheng He. Katika mwaka wa 1498, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri na mvumbuzi maarufu kutoka Ureno, Vasco da Gama.
Karne kadhaa kabla ya ukoloni, upwa wa Kenya wanakoishi Waswahili ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa ya watumwa na pembe za ndovu na Waarabu na Wahindi. Inasemekana kwamba kabila la Wameru lilitokana na watumwa waliotoroka utumwa Uarabunimiaka ya 1700. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitoka milki za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatoka Unguja (kama Tippu Tip)
Itaendelea............
Imeandaliwa na: Mwangazanews
Kwa msaada wa tovuti
Mbali mbali.

EmoticonEmoticon