Je,umekuwa ukipata shida ku_download video za facebook? Kama jibu ni ndio basi leo nimewaletea ujanja na ni rahisi kutumia.
Smartphone zote zinazotumia mfumo wa Android huwa zinakuja na application ya chrome, ni application ambayo inamilikiwa na Google, ili uweze ku_download video yako uliyoipenda kutoka facebook,bonyeza application yako ya chrome ikishafunguka andika facebook kisha tafuta,baada ya facebook kufunguka itakutaka uingize email au namba ya simu pamoja na namba ya Siri unayoitumia
kwenye akaunti yako ya facebook kisha utamalizia na kitufe cha kutafuta, akaunti yako ya facebook ikishafunguka ingia kwenye uwanja wa ku_search(kutafuta) andika jina la ukurasa au akaunti ya mtu ambaye unataka ku_download video aliyoitupia facebook,ukishaipata bonyeza kitufe cha play kwenye hiyo video na ikishaanza kucheza kulia utaona mshale umeangalia chini,utaubonyeza huo mshale kuruhusu program ianze ku_download(kupakia),ikimaliza kupakia utaona Alama ya tiki upande wa juu kabisa wa screen yako,pia application ya chrome inatabia ya kuhifadhi vitu vyote ambavyo una_search kupitia kwake, leo tuishie hapo.
Usikose kufuatilia
Blog ya Mwangaza News
Kwa Habari,Teknolojia na
Makala mbali mbali.
Mawasiliano:
(WhatsApp+255762588445
+255655588445)
EmoticonEmoticon