Jumamosi, 24 Juni 2017

WENYE ROHO MBAYA KAMA HAWA KWETU WAPO WENGI SANA SIJUI KWENU

Tags


Kabla mahusiano yao hayajakolea
jamaa akamkalisha chini huyu mdada na kumpa misimamo yake.

"Mpaka tumekuwa kwenye mahusiano maana yake nimekupenda
Nilikwambia tangu awali nina mke na watoto.
Nampenda mke wangu ndio maana nilifunga nae ndoa.....

Sitamani hata siku moja aje kuumia eti kwasababu yako

Sina malengo yoyote na wewe hususani ya kindoa maana tayari niko na ndoa.....nakuheshimu pia kwa nafasi yako lakini kuwa na nidhamu kwenye ndoa yangu......kukupenda wewe haina maana kwamba mke wangu simpendi no,ni udhaifu wa wanaume tulionao

Sitaki uwasiliane na mke wangu hata mara moja
Sitaki ajue nina hawara nje,mke wangu anasali anamuomba Mungu.

Hata mahusiano yetu najua ataonyeshwa kwenye ndoto tu!
Ni afadhari akawa ana hisia tu lakini sio ajue.

Aisha akajibu " ina maana huna malengo kabisa na Mimi
Ko una mpango wa kunichezea tu?

"Kwani ulitaka nini ziada kutoka kwangu?jamaa akamuuliza.
Nataka unizalie watoto namimi nataka ndoa hata mke wa pili

Haa eti nini!?kama ni hivyo tuishie hapa ,dini yetu hairuhusu kawatafute wakina mzee Yusufu sihitaji stress ndio maana nimekwambia mapema misimamo yangu kama utaiweza,huiwezi tuishie hapa....

Haya nimekuelewa ntafuata huu utaratibu kwasababu nakupenda.alijibu dada.....poa una amani lakini?aliuliza jamaa
Yes usijari......

Naomba ninapokuwa nyumbani usinitext wala nisiione call yako ni mpaka iwe ninapokuwa kazini tu.....

He sasa si uweke password kama hutaki mkeo asione simu yako?
Hapana sitaki kuonekana kutokuaminiwa na wife...na usichati na Mimi kwa msg za kawaida au Whatsap wala messenger,tutumiane email tu.

Aisha akajibu "sawa"

Uhusiano wao uliendelea lakini Aisha hakuwahi kuwa na amani kwa mapenzi yenye mashart kama yale ,ilikuwa inamuuma akikumbuka maneno ya jamaa na vile anavyo mheshimu mkewe na si yeye.....alivumilia tu kwakuwa jamaa ana hela,chochote alichotaka alipewa.

Alitumia kila mbinu ili kumvutia jamaa,alijaribu kumuuliza kitu anachokipenda huyo buana ili amfanyie mfano chakula anachopenda,lakini jamaa hakuwa muwazi Sana kwake.

Alitamani sana kumjua huyo mke wa jamaa lakini hakuweza
Alijaribu kutafuta hakufanikiwa,ila mara kadhaa alimskia jamaa akiongea nae kwenye simu anamuita Magdalena.....au mama Francisco.

Siku moja akiwa saluni kwake aliyofunguliwa na jamaa akiwa na msichana wake wa kazi
Akaanza kupitia Facebook akaingia kwenye profile ya jamaa aone marafiki zake ,

Akasearch jina la Magdalene akalipata,akafungua profile yake akakuta ni kweli ni mkewe jamaa,kwanza alimuweka mumewe Picha yake ya wasifu.

Akamuomba urafiki,muda huo huo mag akaacept......akamshukuru kwa kumkubalia urafiki mag akamwambia "karibu my"
Akajibu asante....

Wakachat sana siku ile.....huyu Aisha akajisemesha "nimemmaliza tayari.....usiku ule hakulala usingizi akimtafakari yule mwanamke....amfanyie nini maana ndio kikwazo kikubwa chake.

Kulipokucha mchana akiwa nyumbani kwake akamtext msichana wake
" nimeongea na huyu mshamba nimemkaribisha saluni nimemwambia tunampa ofa aje,sasa naomba akija hapo wewe endelea kumfumua hizo nywere zake Mimi nitamnunulia soda ntamuwekea na pilipili atajuta kunifahamu"!

Dada pilipili!!?aliuliza huyo binti
Wewe nawe baki na hilo ilo ,namaanisha sumu!alijibu Aisha
Anhaà hapo sawa,ko nisimuwahishe niende nae taratibu?

No wewe Fanya kawaida Mimi dakika chache ntakuwa hapo...alijibu aisha

Mag dakika 20 akawa amefika na gari yake
Akamjulisha Aisha akampa maelekezo msichana wake akawa amemwona akampokea.....wakaanza kazi

Dakika 10 mbele Aisha akawa amefika ,story zikaendelea
Magdalene hamjui Aisha, Aisha anamjua Magdalena.

Baada ya kumsuka nywere akiwa karibu na kumaliza Aisha akamwambia ngoja nikununulie na soda japo ukanywe hata nyumbani,soda gani vile?

"Yoyote nichukulie my dear nashkur sana"alijibu mag

Aisha akazuga kama anaenda dukani lkn alikuwa kazunguka nyuma ya saluni yake akatoa chupa ya take away kwenye pochi yake, na akapita dukani akaagiza zingine mbili za kwao na binti yake.

Akampa Magdalena soda aina ya pepsi,akashukuru akawasha gari akaondoka.....akionyesha kufurahishwa na Huduma zao na upendo au ukarimu wao asijue mtego wa muwindaji.

Huku nyuma walianza kupongezana wakiamini zoezi lao limefanikiwa walijua kwa vyovyote vile angekunywa njiani
Na iwapo angekunywa tu asingefika mbali kutokana na ujazo wa paketi aliyomimina kwenye chupa......

"sikutaka kumpa mapema halafu afie hapa sitaki mizoga ya watu hapa akafie mbele huko pumbavu kabisa" alijisemesha Aisha.

Kumbe Magdalena ile soda hakunywa kwenye gari.

Akawa amefika nayo mpka home.....

na kwasababu ilikuwa imepoa akaingia nayo ndani akaiweka kwenye friji akazichanganya na zingine.

Ikawa imelala kwenye friji.

Mchana wa kesho yake jamaa akarudi nyumbani kula chakula
Alipokuwa anaondoka kurudi ofisini,akamwomba mkewe ampe soda,na soda yake kubwa ni pepsi akampa ile ya kina Aisha pasipo kujua .

Patamu hapo......

Akiwa anaondoka akaona kuna email imeingia ,kucheki anakutana na text ya Aisha "uko wapi my?"

Natoka nyumbani naenda ofisini, OK basi nipitie saluni Nina shida kidogo..........

Anataka amuulize maendeleo ya familia yake ,ana wasiwasi je soda ilinyweka?au ile sio sumu kadanganywa?

Jamaa alipofika Aisha akaingia kwenye gari akamkiss jamaa
Wakaondoka wote kuelekea ofisini kwa jamaa.

Aisha akalalamika njaa ikabidi ampitishe mahali akala akamsubiri.
 walipokuwa wakiondoka akiwa kwenye gari akaona soda akamwomba anywe,jamaa bila ajizi yoyote akampa....kumbe ni ile yenye pilipili!

Na kwakuwa alikuwa kakaukiwa akaanza nayo hapo hapo!
akakata kama nusu hivi

Huku wakipiga story........

Dakika tano peke zilikuwa ni nyingi akaanza kuskia maumivu makali hamna mfano,moja kwa moja akajua ni ile soda.....ha! Akajishika tumbo akatoa macho akamuuliza "hii umeitoa wapi?jamaa akajibu" nyumbani kwenye friji langu"

Ooooooh my god mkeo ameniua jamani! Mkeo ameniua niwahishe hospital plz!

Mke wangu amekuua?
kivipi hebu niambie!!!

Dah!Kweli mkeo anasali.......
Aisha anaongea huku akilia kwa uchungu mkubwa akatamka neno la mwisho akasema
"Nakufa kwa upumbavu wangu mwenyewe, niwahishe hospital labda ntapona mimi!

Jamaa dakika 15 akawa amefanikiwa kufika hospital akaingia nae ,jopo la madaktari wakiwa wanamhangaikia yeye akawa amewasha gari akatoroka kukwepa msala.......huku nyuma Aisha ikawa ndio kwa heri bye bye!

Kuchunguzwa ikaonekana amekufa kwa kula chakula au kinywaji chenye sumu.

Kumtafuta aliyemleta hospital wakashangaa hawamwoni.na bahati nzuri simu ya marehemu akawa ameondoka nayo.

Taarifa ikafika police.

Na ilipotangazwa iwapo angetokea ndugu wa marehemu ,wa kwanza akawa ni binti wa saluni.

Police ilibidi waanze nae yeye kuchunguza simu yake,Bahati nzuri au mbaya kwake,zile Meseji walizochati na dada hakuzifuta.........

binti akawa ni mtuhumiwa namba moja ilionekana kuna MTU walimpa sumu na marehemu lakini ninani?na mbona Aisha ndiyo amekufa tena?wakaenda kuirenew ile line ya marehemu.

Upelelezi ulipokuwa ukiendelea tayari yule binti akabanwa mpaka akakiri kuhusu mpango waliousuka na marehemu dhidi ya mke wa jamaa aitwaye japhert..... Walipomtafuta akaja japhert pamoja na mkewe.

Magdalena akahojiwa kama anamfahamu Aisha akaeleza vile walivyojuana kupitia Facebook kama wiki tatu tu.

Akaeleza vile walivyompa na ofa ya kwenda kusuka na
"huyu binti ndiye aliyenisuka na wakaninunulia soda" lakini ile soda sikuinywa nikaenda nayo nyumbani.....................akasimulia kama hapo juu.

Mume akawa anashangaa anaona ni kama move baadae mahakama ikamtia hatiani yule binti.

Walipofika nyumbani Magdalena ilibidi ambane mumewe

"Vipi Mume wangu marehemu kumbe alikuwa hawara wako?"
Ilibidi mumewe awe muwazi tu kwake,akamweleza Kisa kizima
huku akilia kwa uchungu mkubwa.......

Ni kweli Mimi ndio nilitaka kukuua kwa upumbavu wangu,naomba unisamehe,sijui kwanini wanaume haturidhiki na hatutosheki?hakuna chochote ninachokikosa kwako lakini tamaa tu!

Usimwache Mungu unayemtumikia mke wangu,ningefanyaje Mimi kukupoteza wewe!?

ningefanyaje na watoto hawa?
Mama akamfuata mkewe akamkumbatia miguu huku akilia
Jamaa akawa ameishiwa maneno ya kuongea zaidi ya "nisamehe".......wakaangua kilio cha kumshukuru Mungu.

Mwishoni mama Francisco akiwa amemkumbatia mmewe,anasema mwili wote ulikuwa kama unachemka,akasema nyamaza nimshukuru Mungu:

"EEH MWENYEZI MUNGU,BABA WA REHEMA,MUNGU UTULINDAYE,
BIBLIA IMESEMA WEWE USIPOULINDA MJI WAULINDAO WAKESHA BURE.......

USIPOILINDA NDOA,HATUWEZI KUFANYA CHOCHOTE.......

ASANTE KWA UAMINIFU WAKO KWANGU,
ULINIAHIDI IWAPO NIGEKUWA MWAMINIFU KWAKO,USINGENIACHA WALA KUNIPUNGUKIA HATA SEKUNDE TANO!

NA KWAMBA MAADUI ZANGU WANGEKUWA ADUI ZAKO.
NA UMESHATIKIZA AHADI YAKO KWANGU.

ASANTE KWA KUHAKIKISHA NAZIDI KUWA SALAMA.
UMETULINDA MIMI NA MUME WANGU NA WATOTO.

ILE SODA PAMOJA NA KWAMBA IMEINGIA MPAKA NDANI KWANGU,LAKINI HAKUNA ALIYEKUNYWA NAJUA NI UWEZA WAKO LAKINI HATA MMOJA WETU ANGEKUNYWA ASINGEDHURIKA MAANA UMESEMA " TUKILA VYA KUFISHA HAVITATUDHURU............TULINDE TUTUNZE ZAIDI KWA UTUKUFU WA JINA LAKO AMENI.

Baba Francisco yupo ametulia na mkewe sasa hivi na ameshika sana mambo ya imani,anasali balaa.

Anajuta kwanini alijiingiza kwenye matatizo eti kwasababu ya hawara.......hataki kabisa kuisikia michepuko.

Nasema hivi tenda wema UTAVUNA mema
Ukitenda kwa hila UTAVUNA hila.

By Kuhani Mlawi

Jumatano, 21 Juni 2017

MAJONZI MAKUBWA KATIKATI YA FURAHA

Tags


Baada ya jamaa kutangaza uchumba na dada mmoja, kumbe dada mtu anamfahamu vizuri sana huyu mchumba wa kaka yake ambaye ni wifi yake na wamesoma wote secondary kidato cha kwanza mpaka cha nne lakini walipotezana miaka mingi.

Ilikuwa ni ijumaa moja ambapo jamaa aliamua kumpeleka kwa wazazi wake,na alikwisha waandaa wiki moja nyuma, kwa hiyo walikuwa wamejiandaa akiwepo na wifi japo mpaka hapo hakujua ni MTU wa aina gani anaekuja kutambulishwa.

Ilikuwa majira ya saa 7 jamaa na mchumba wakawa wameshatia timu nyumbani kwa baba na nama.

Walipoingia tu ndani ya geti dada mtu akachungulia kupitia dirishani amwone wifi yake,akashangaa kumwona Beatrice waliesoma wote. gafla akawa amekasirika vibaya mno akikumbuka historia ya mwenzie huyo haikuwa ni nzuri miaka hiyo ya nyuma.

Walipoingia ndani sebuleni familia nzima wakamkaribisha kwa furaha mgeni kasoro veronica alikuwa amekosekana sebuleni akawa amejifungia ndani.....

alipogongewa akatoa udhuru kana kwamba tumbo limechafuka ghafula lakini angetoka baada ya dakika chache,lakini kusema ukweli alikuwa amelala anachati na marafiki zake kupitia group la whatsap la wanafunzi wenzake waliomaliza pamoja akimkejeri kaka yake kwa uamuzi wa kuoa mtu ambaye alishawahi kubakwa na wanaume zaidi ya 6

basi wenzie walianza kutuma katuni😂💇😷 za kuonyesha kumlilia kumsikitikia huyo brother.....

"Heheheeeee ngoja niende sebuleni nikamwone wifi jamen!!!aliwaaga wenzie group wengine wakamjibu " atashtukajee!!!

ataona aibu huyoo! Anataka kumwuua kaka wa sie!!tena hawezi kukosa kuwa na magonjwa huyo. Alijibu mmoja wa marafiki zake.vero akazima data.

Basi walipokuwa wapo karibu na kumaliza vero akatoka akiwa amenuna akafika sebuleni.

He!wewe ni veroo! Waoo rafkiang!!

alisema kwa furaha Beatrice akisimama kwenda kumuwao vero,lakini vero alikuwa kawaida tu akamsalimia na kukaa........kile kitendo kilimuudhi kaka yake akamuuliza mchumba wake,

"Unamjua vero?

Yes tumesoma wote alipokea Beatrice.

Akapokea baba " wewe vero kumbe unamfahamu WiFi yako mbona huonyeshi kufurahi?

Hapana baba mbona nimefura tu!!karibu sana wifi tunakupenda alijibu vero

"Asante sana mwe nimefrahi kumbe wewe ni WiFi kweli Mungu ana makusudi, tulikuwa marafiki shuleni lakini sasa ni zaidi ya rafiki hakika Mungu ni Mkuu! Alisema Beatrice kwa Furaha.....vero hakuwa mwenye Furaha kusema ule ukweli.

Basi walipomaliza ,wakataka kutawanyika,Beatrice akasema akaomba kusema kidogo.

"samahani sana baba na mama na WiFi yangu na shemeji zangu kwa kunikaribisha ,sina mengi ya kusema na samahani kwa Uhuru wangu wa kuwa msemaji wakati sio vizuri sana kuwa msemaji sana kwa wakwe zako ,nafikiri nimeshindwa kuzuia Furaha yangu hasa nilipomuona vero,tulipotezana kama miaka 6 hivi hata kimawasiliano........kuna vitu vingi vibaya tulivifanya wakati huo kwa sababu ya ujana ulikuwa ni mwingi....

Akamgeukia vero na kumwambia "kwasasa sio yule wa miaka ile
Nimeokoka nampenda Mungu......amenifanya kiumbe kipya......
Beatrice akaanza kutokwa na machozi sijui alikumbuka nini.
Nafkir alikuwa anajua fika kwamba vero atavuruga uhusiano wao kutokana na hali aliyoiona pale sebuleni.

Basi mchumba wake akamkumbatia akawa anampiga kifuani akaanza kulia nae,wazazi hawakuwa wanaelewa kinachoendelea
Vero anajua kinachoendelea
Beatrice anajua kinachoendelea

John anajua kinachoendelea,maana historia yote mchumba wake alishamwambia mapema,vile alivyowahi kubakwa alipokuwa na rafiki zake moja ya fukwe za bahari.

 week end moja walienda beach wenzie wakaingia baharini kuogelea lakini yeye alikuwa anaogopa,baadae kuna vijana wakamshawishi kuingia kwenye tube moja la kuogelea wakimwambia hawatampeleka mbali,basi alipoingia tu,wakampeleka kwenye kina kirefu ambako walimfanyia upuzi wote huko hasa wakitumia vidole......alijaribu kupiga kelele lakini kwenye maji sauti haifiki mbali.......

Wenzie walipotoka nje kama saa 11 jioni akiwemo na vero walipomkosa hawakujari,walichojua ameamua kuondoka lakini kumbe mwenzao yuko majini wakawa wameondoka eneo hilo.

Beatrice Kule majini akawa hali mbaya kalipoingia kagizagiza wakaamua wamtoe nje na kumbaka kwa kupokezana na akawa amepoteza ufahamu, wakamwacha ,baadae wasamalia wema wakaita police wakamkimbiza hospital na akawa ameshonwa kutokana na kumchana sehemu za siri na waandishi wa habari wakamchukua Picha na kesho yake ikatoka habari ile na picha zikachukuliwa.

Taarifa zikawafikia ndugu wakafika hospital Beatrice alipopata fahamu police wakachukua maelezo yake wakagundua kuwa mara ya mwisho alikuwa na wenzie [wakina veronica] wakaenda kuchukuliwa na kuwekwa ndani lakini baadae walikuja kuachiwa kwa dhamana,ni story ndefu mimi naenda kwa kifupi.......

Beatrice akiwa amekumbatiwa na mchumba wake wakilia,baba akawauliza KWANINI MAJONZI MAZITO KATIKATI YA FURAHA?

John akasema"nakupenda kuliko chochote dear wewe unamcha Mungu,biblia inasema  usiyatafakari mambo yaliyopita maana Mungu ni wa mambo mapya siku zote......

niko tayari kulia na wewe na kufurahi na wewe siku zote....

akachukua kitambaa na kumfuta mchumba wake.

"Asante my alijibu Beatrice.
Akachukua hicho kitambaa akamfuta john
Thanks, alijibu john.

Baada ya hapo Beatrice mwenyewe akasema naomba nimshukuru Mungu kwa siku kubwa kama hii,wote wakafunika macho.

"Mwenyezi Mungu Baba wa rehema
Asante kwa kutukusanya leo na familia hii,
Nakushukuru kwa kunipenda na kunithamini
Umenistahilisha wakati nilikuwa sistahili
Laiti kama ungelihesabu makosa yetu tusingekuwa na ujasiri wowote wa kusimama mbele zako wala kuomba chochote......tunapotoka mahali hapa,ulinzi wako uwe nasi amen!wote wakaitikia amen!

Wakakumbatiana lakini wakati akiwa anaomba vero alikuwa ameshatoka na kuingia chumbani kuchati na marafiki zake kuwapa feedbacks....

Wanapoagana Beatrice akasema naomba mniagie WiFi yangu mama,mama akajibu "naona ako na mchafuko wa tumbo kidogo aliongea ili kumtetea tu.

Baba na mama na watoto waliporudi ndani ,wakamwita vero sebuleni wakitaka kujua nini anachojua kuhusu WiFi yake.

Siwezi,siwezi,nasema tena siwezi narudia tena kusema siwezi kumuunga mkono john kumwoa yule msichana ,eti anajifanya mlokole,mnafki mkubwa tu yule malaya,akaeleza mambo chungu nzima kumhusu Beatrice.......oneni wenyewe hii simu muone hata marafiki zangu wanavyomjua ana history chafu.....

Mdogo wake mmoja akachukua ile simu aone chatting za group

Mbona hizi chatting zole ni za nyuma lakini unajuaje labda kabadirika? Alisema huyo dogo.

Kabadirika wapi!?hakuna mwanamke palee!!alijibu vero

Baba akachukua aone nae
Ha!kumbe huyu ndiye yule binti ambaye alibakwa kipindi kile wewe nakuhangaikia police? Ndiyo baba nakumbuka ulitoa hela nyingi sana ili Mimi nitoke halafu eti ndiyo aolewe tena na kaka!?
Ametoa mimba nyingi sana Beatrice Mimi namjua ndio maana aliponiona alishtuka na kuanza kulia

Baba akamuuliza vero" kwani Beatrice alipenda kubakwa?

Huoni kama ninyi pia mlichangia kubakwa kwake?

Hii ilikuwa ni ngumu sana kwenu iwapo angekufa yule binti maana ilionekana mmeenda kumtelekeza mwenzenu kule......lakini nilienda kwa wazazi wake wakatusamehe na ilikuwa nitoe pesa za matibabu lakini wakakataa........nafurahi kwamba tunarudi tena kwao najua tunakwenda kuwapoza maumivu ya binti yao.

Vero alitaka aendelee kubisha mzee akamchapa kibao,pumbavu!,nyamaza,acha wivu na roho mbaya......vero akaamua kuondoka pale sebuleni........ Njoo hapa upesi! Mzee alimwita
"Sitaki!alijibu kwa hasira!
" sawa mwanangu mavuno yako yapo.....alijibu baba kwa upole.

"Hakuna shida,na nawaambieni akimwoa huyo msichana sintokuja kukanyaga kwake, wala harusini nisishirikishwe chochote. Alijibu tena vero.
Mama akapokea " hata usipokuja kwani Mungu anakutegemea wewe ili kufanikisha shughuli hii?Mungu ana watu wengi Mwanangu! Ila wewe unajifungia mlango maana wewe mwenyewe umeshachumbiwa tayari......sasa ukiendelea na hiyo tabia utavuruga mipango yako.......jaribu kufkir kama mchumba wako angeambiwa habar ya kiburi ulichonacho utaolewa kweli??

Kumbe mmoja wa marafiki zake alitunza kipande cha gazeti ambalo liliandika tukio la Beatrice, vero akafight mpaka akakipata na kwenda moja kwa moja kumpelekea john ili ajionee mwenyewe

Akampigia simu iwapo kama alikuwepo nyumbani, john akasema ndio karibu.......alipofika akachomoa kwenye pochi yake kipande cha gazeti na kumpa brother.......john kuangalia akakutana na kichwa cha habari chenye maandishi makubwa

BINTI ABAKWA HADI KUZIMIA UFUKWENI NA VIJANA ZAIDI YA 6 ----------------------------------++++++++++++++-------------------------------------------------\\\\\\\
Hicho kichwa cha habari kiliambatana na Picha ya Beatrice akiwa katika hali mbaya...........brother aliinama mezani na kuweka kichwa chake kwenye lile gazeti alilia sanaa kama dakika 20 huku vero akiamini sasa lengo lake limefanikiwa.......

Alipojiinua kipande cha gazeti lote kilikuwa lishalowa na machozi yake,

Aah mbona umelowanisha kabla hujasoma habari yote!!?alijibu vero huku akikichukua kile kipande,lakini john akamalizia kabisa kuchana......hivi ninavyochana ndivyo Mungu anavyozifuta history zetu chafu tunazopitia maishani ila mwanadamu hawezi kusahau.....ninachotaka kukwambia ni kwamba;

Achana na mambo ya watu wengine yasiyokusaidia chochote!

john huyu mwanamke atakuua ni mgonjwa!
Halafu ni mkubwa kwako!!alisema vero

Tumepima yuko salama hana tatizo
Hii story iliyopo kwenye gazeti alishaniambia kitambo iwapo ningekuwa tayari kuoa mwanamke wa aina yake....nilikubali.
Namimi nikamsimulia ya kwangu akasema yu tayari....miaka yake anaijua amenizidi mitatu lakini wangu sio shida,najua ana watoto wawili nje ya mimi lakini nimempenda pamoja na hao watoto wake,na ntamsaidia kuwalea.

Dada,bidii uliyotumia kutafuta hili gazeti,Kama ungeitumia kutafuta kazi ili elimu yako iwaletee matunda wazazi waliotusomesha,pengine ungekuwa kazini tayari.......

huyu vero alishachafuliwa sawa,lakini Mungu kamsafisha tayari ila wewe unataka kuanza kwa upya kumchafua tena,Mimi nakwambia humchafui yeye ila unanichafua mimi na familia yetu kwa ujumla,na huna usalama wowote kama ukiendelea na hiyo tabia dada.......Beatrice nilimpenda,nampenda,na nitaendelea kumpenda,na sintorudi nyuma kamwe! Huyu ndiye niliyepewa na Mungu.

Sijawahi kukusimulia history ya maisha yangu kwa muda ambao nimekaa mbali na wazazi wangu hata wewe hujui chochote na laiti kama ungenijua usingeendelea kumchafua Mtoto wa watu.....

Mimi nimefanya vitendo vya ujambazi vingi sana,nimemwaga damu nyingi za watu wasiokuwa na hatia lakini nimebadirika na Mungu amenisamehe japo nilijaa na lasna ya damu za watu,,,,,,nani angependa kuolewa na jambazi?

nashangaa unaniona kama malaika eti Beatrice hafai na hana sifa ya kuolewa namimi,,,,,,,,nasema hivi ,mimi ndiye nisiye na sifa ya kuwa Mume wa huyu mwanamke,lakini Mungu amenistahilisha.........

Baada ya hayo maneno ,Beatrice akawa anaingia,vero alipomwona akatoka kwa speed wakakutana mlangoni bila hata salamu

WiFi kulikoni? Beatrice alimuuliza
Vero hakujibu
Akaingia ndani akamkuta john nae ana alama za machozi mashavuni......dear umemfanya nini WiFi mbona analia
Hapana hakuna kitu dear sijui ana shida gani.....

Veronica akatoka nje akaita Bodaboda akamwambia Dereva nikimbize haraka sana usipunguze mwendo nipeleke nyumbani......

Walipokamata barabara muda wote Veronica alikuwa anajisemesha njiani......hasira zote ziliishia kwa Dereva akimfokea kwa kuendesha pikipiki taratibu......Dereva akaongeza mwendo ile anaovertake gari moja la mizigo pikipiki ikamiss akataka kutoka nje ya barabara bahati mbaya  akakumbana tax wakapigwa vibaya vero ndiye alikuwa kaumia sana akavunjika miguu yote miwili mmoja ulikatika juu ya goti mwingine ulivunjika chini kabisa sehemu kuvaa kiatu na waliseleleka na ile pikipiki ikawa imemchubua uso upande wa kushoto akawa kama ameungua.......ilikuwa ni MAJONZI makubwa lakini uzuri wake hakufa.

Ilipita miaka miwili akawa amepona ila alikuwa tayari hana Miguu ,naye alikuwa na mchumba wake akawa amemwacha kulingana na hali aliyokuwa nayo,ila kabla hajamwacha akawa amemnunulia Miguu ya bandia na ndiyo zawadi aliyomwachia.

Katika miaka miwili ambayo vero alikuwa anaugua, john na Beatrice walifanikiwa kufunga ndoa ilikuwa ni ya baraka sana haikuwa na mfano kutokana na wengi walivyomjua Beatrice wakaja kushuhudiavtukio ambalo mke na Mume wanapendana sana......

Dakika chache tu kabla john hajaenda kufunga ndoa,rafiki zake watumishi wakamwombea ili aendako aende salama......

Na tayari wana watoto wawili Enes wakike ndiye mkubwa na wapili ni wa kiume anaitwa innocent.

Nakumbuka tu maneno ya baba kwa vero
"MAVUNO YAKO YAPO MWANANGU".

Kitu cha kujifunza zaidi,kabla hamjaanza mahusiano na huyo mwenzio,muweke wazi kila kitu kihusucho maisha yako ya nyuma ,usimfiche.
Kama una watoto.
Miaka yako.
Ulishawahi kuoa au kuolewa?
mwambie ukweli maana ukimficha atakuja kujua tu,na hii ndiyo ilimsaidia Beatrice.....

KUWA MAKINI NA UNACHOPANDA SASA MAANA UTAVUNA TU HAPA HAPA DUNIANI.


By Kuhani Mlawi

Jumatatu, 19 Juni 2017

Historia ya nchi ya Kenya, nchi ambayo itafanya uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge hivi karibuni-01

Tags

Historia ya Kenya inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kenya.

Historia ya awaliEdit

Uvumbuzi wa majuzi karibu na Ziwa Turkana unaonyesha kwamba kiumbe kama Australopithecus anamensis aliishi katika eneo ambalo sasa ni Kenya kuanzia miaka milioni 4.1 iliyopita.
Lakini mabaki yaliyopatikana katika mabonde ya Tugen, yaliyokuwa na takriban miaka milioni 6, yalipelekea kutajwa kwa aina mpya ya spishiOrrorin tugenensis.

Ustaarabu wa mapema KenyaEdit

Mahali pa Msikiti Mkuu wa Gedikarne ya 13.
Wakushi kutoka Afrika kaskazini waliingia eneo linaloitwa Kenya miaka ya 2000 KK.
Katika milenia ya 1, wazungumzaji wa lugha za Kinilo-Sahara na lugha za Kibantu waliingia katika eneo hili, na sasa Waniloti ni 30% ya Wakenya wote. Pwani ya Kenya ikawa makao ya jamii ya wahunzi na jamii ya wakulima wadogo wadogo, wawindaji na wavuvi ambao walikuwa mhimili wa uchumi kwa kushirika katika kulimo, uvuvi, utengenezaji chuma, na kufanya biashara na nchi za kigeni.
Kuanzia karne ya 6 au karne ya 9, Kenya ilijihusisha na shughuli za ubaharia kukuza uchumi ikaanza kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.
Wafanyabiashara Waarabu walianza kwenda pwani ya Kenya mara kwa mara karne ya 1 BK. Kenya ilikuwa karibu na Peninsula ya Arabia na hii ilialika ukoloni.
Makazi ya Waarabu na Waajemi yaliongezeka kandokando ya pwani kufikia karne ya 8. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa machotara, Waafrika-Waarabu.
Kuanzia karne ya 6 au karne ya 9, Kenya ilijihusisha na shughuli za ubaharia kukuza uchumi ikaanza kutengeneza meli za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye bandari kama Kilwa na Shanga iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.
Mombasa ulikuwa mji wenye bandari wa nchi ya Kenya kabla ya ukoloni katika Enzi ya kati. Bandari hiyo ilitumika kuendeleza biashara na miji mingine yenye bandari Afrika, Uajemi, na wafanyabiashara Waarabu, Yemeni na hata Bara Hindi.
Baharia Mreno Duarte Barbosa wa karne ya 15 alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi, mashua nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutoka Sofala na nyingine kutoka CambayMelinde na nyingine zinazoabiri hadi kisiwani Unguja."
Kiswahili, ambayo ni lugha ya Kibantu iliyokopa misamiati ya KiarabuKiajemi na mingine kutoka Mashariki ya Kati na Asia Kusini, baadaye ilikua ikawa lingua franca ya kibiashara kwa jamii mbalimbali.
Kwa karne nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya ni mji wa Malindi. Umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangu karne ya 14 na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwa serikali zingine.
Mwaka wa 1414Sultani Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Uchina wa Ming, wakati wa safari za mchunguziZheng He. Katika mwaka wa 1498, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri na mvumbuzi maarufu kutoka Ureno, Vasco da Gama.
Karne kadhaa kabla ya ukoloni, upwa wa Kenya wanakoishi Waswahili ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa ya watumwa na pembe za ndovu na Waarabu na Wahindi. Inasemekana kwamba kabila la Wameru lilitokana na watumwa waliotoroka utumwa Uarabunimiaka ya 1700. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitoka milki za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatoka Unguja (kama Tippu Tip)
Itaendelea............
Imeandaliwa na: Mwangazanews
                               Kwa msaada wa tovuti 
                               Mbali mbali.


Edi



Edi