Rais wa Marekani Donard Trump amesema atatumia jitihada zake zote kulejesha na kufanyikisha mazungumzo ya Amani kati ya Israel na Palestina.
Kauli hiyo ya Trump ameisema baada ya kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Bethlehem katika eneo la ukingo wa magharibi.
Rais Donard Trump (Kushoto) alipokuwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas (Kulia) leo Mei 23,2017 pic. Reuters.
Israel na Palestina hazijakutana kwa mazungumzo ya kutafuta Amani kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo Sasa.
Trump amesema kuwa kufanyikisha kwa mazungumzo hayo ni Kazi kubwa na ni ngumu sana.
Pamoja na hivyo, amesema hatua ya kwenda Mjini Bethlehem na kukutana na Abbas ni ishara ya kuleta mwafaka.
''Nitajaribu kuleta Amani kati ya Wapalestina na Waisrael nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kwa kufanyikisha Jambo Hilo" alisema Rais Trump.
Baada ya kukutana na Rais Abbas, Trump ambaye anamalizia ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati hivi leo amerejea Mjini Jerusalem kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Donard Trump amesema uhusiano Kati ya Marekani na Israel hautaweza kuvunjika na Mataifa hayo mawili yataendelea kushirikiana katika maswala ya Usalama na kuushinda ugaidi.
"Serikali yangu itasimama siku zote na Israel"Rais Trump alisema hayo akiwaambia Waisrael.
Na baada ya kumaliza ziara yake Nchini Israel, Trump ataelekea Nchini Italia kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis mjini Vatican.
Siku ya Ijumaa na Jumamosi, Trump atahudhuria mkutano wa nchi zenye utajiri wa viwanda wa G7 mjini Taomina Nchini Italia.
EmoticonEmoticon