Home
Archives for Mei 2017
Jumatano, 31 Mei 2017
JINSI KUNDI LA RICH GANG LILIVYOMWAGA PESA KWENYE KABURI LA IVAN SSEMWANGA (VIDEO)
Diterbitkan Mei 31, 2017
Tags
SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JOB NDUGAI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MWENYENYEKITI WA CHADEMA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA MOSHI MJINI
Diterbitkan Mei 31, 2017
Tags
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano was Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amemtumia salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mheshimiwa Freeman Mbowe kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo LA Moshi Mjini 2000-2015,Mheshimiwa Philemon Ndesamburo kilichotokea leo Mkoani Kilimanjaro.
Jumanne, 30 Mei 2017
Ivan kuzikwa leo, Zari aahidi kuwaangalia watoto
Diterbitkan Mei 30, 2017
Tags
Baada ya Jumatatu mwili wa Ivan Ssemwanga kuangwa na kufanywa ibada takatifu,aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu,Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza.
Katika miss ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Namirembe mjini Kampala Uganda, Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.
Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhulia walijiandaa kumsikiliza atakachosema.
"Sitomhuzunikia Ivan"alisema.
"Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu tulitengana kwa sababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan.
Ivan alijua kile ninachoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua ningewaangalia vijana vyema na aliniamini.
Kwa hali hiyo,ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye."
Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili nae aliahidi kuhudhuria.
Source:bongo5.com
Jumatatu, 29 Mei 2017
Jumatano, 24 Mei 2017
Jumanne, 23 Mei 2017
TRUMP ASEMA ATATUMIA JITIHADA ZAKE ZOTE KULETA AMANI KATI YA ISRAEL NA PALESTINA
Diterbitkan Mei 23, 2017
Tags
Rais wa Marekani Donard Trump amesema atatumia jitihada zake zote kulejesha na kufanyikisha mazungumzo ya Amani kati ya Israel na Palestina.
Kauli hiyo ya Trump ameisema baada ya kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Bethlehem katika eneo la ukingo wa magharibi.
Kauli hiyo ya Trump ameisema baada ya kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Bethlehem katika eneo la ukingo wa magharibi.
Rais Donard Trump (Kushoto) alipokuwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas (Kulia) leo Mei 23,2017 pic. Reuters.
Israel na Palestina hazijakutana kwa mazungumzo ya kutafuta Amani kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo Sasa.
Trump amesema kuwa kufanyikisha kwa mazungumzo hayo ni Kazi kubwa na ni ngumu sana.
Pamoja na hivyo, amesema hatua ya kwenda Mjini Bethlehem na kukutana na Abbas ni ishara ya kuleta mwafaka.
''Nitajaribu kuleta Amani kati ya Wapalestina na Waisrael nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kwa kufanyikisha Jambo Hilo" alisema Rais Trump.
Baada ya kukutana na Rais Abbas, Trump ambaye anamalizia ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati hivi leo amerejea Mjini Jerusalem kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Donard Trump amesema uhusiano Kati ya Marekani na Israel hautaweza kuvunjika na Mataifa hayo mawili yataendelea kushirikiana katika maswala ya Usalama na kuushinda ugaidi.
"Serikali yangu itasimama siku zote na Israel"Rais Trump alisema hayo akiwaambia Waisrael.
Na baada ya kumaliza ziara yake Nchini Israel, Trump ataelekea Nchini Italia kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis mjini Vatican.
Siku ya Ijumaa na Jumamosi, Trump atahudhuria mkutano wa nchi zenye utajiri wa viwanda wa G7 mjini Taomina Nchini Italia.
UN WAIOMBA PYONGYANG KUSITISHA HARAKATI ZAKE ZA KUENDELEA NA MAJARIBIO YA KURUSHA MAKOMBORA
Diterbitkan Mei 23, 2017
Tags
Umoja wa Mataifa umeiomba Korea ya Kaskazini "kusitisha mara moja majaribio yake ya Makombora ya masafa marefu ambayo yanahatarisha Usalama wa Kimataifa''.
Kuendelea kwa Korea ya Kaskazini na majaribio yake ya kurusha Makombora ya masafa marefu,"kuna maanisha kwamba Korea ya Kaskazini inapinga Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."
Korea ya Kaskazini imesema Siku ya Jumatatu Mei 22,2017 kuwa ilifaulu kurusha Kombora la masafa marefu ya wastani licha ya kukabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapiga marufuku kujihusisha na kufanya majaribio ya Makombora ya masafa marefu.
Washington pia inafanya mazungumzo na Beijing,mshirika mkuu wa Pyongyang, kuhusu Azimio jipya la kuongeza shinikizo kwa Serikali ya Kikomunisti ya Pyongyang.
Kuendelea kwa Korea ya Kaskazini na majaribio yake ya kurusha Makombora ya masafa marefu,"kuna maanisha kwamba Korea ya Kaskazini inapinga Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."
Raia wa Korea ya Kaskazini wakiangalia kupitia televisheni habari kuhusu urushwaji wa Kombora Mei 22,2017 pic.AFP
Korea ya Kaskazini imesema Siku ya Jumatatu Mei 22,2017 kuwa ilifaulu kurusha Kombora la masafa marefu ya wastani licha ya kukabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapiga marufuku kujihusisha na kufanya majaribio ya Makombora ya masafa marefu.
Washington pia inafanya mazungumzo na Beijing,mshirika mkuu wa Pyongyang, kuhusu Azimio jipya la kuongeza shinikizo kwa Serikali ya Kikomunisti ya Pyongyang.
Jumatatu, 22 Mei 2017
HAYA NAYO NI MAAJABU.
Diterbitkan Mei 22, 2017
Tags
Nchini Misri kinyozi mmoja anatumia Moto kukata nywele.
Source: voaswahili.com
Jumapili, 21 Mei 2017
WACHEZAJI WA TIMU YA MPIRA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI
Diterbitkan Mei 21, 2017
Tags
Klabu ya Mpira Ruvu Shooting,wamepata ajali walipokuwa safarini kutokea Mkoani Shinyanga leo asubuhi.
Timu hiyo ilikuwa safarini ikitokea Mkoani Shinyanga ilipokwenda kucheza mchezo wa mwisho Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Jana dhidi ya Stand United,taarifa zinasema ajali hiyo imesababisha majeraha madogo madogo kwa baadhi ya wachezaji na Basi lililokuwa limewabeba kuharibika vibaya.

Jumamosi, 20 Mei 2017
Mwangaza news blog sasa ipo hewani
Diterbitkan Mei 20, 2017
Tags
Karibu mwangaza news, hapa utapata habari za kweli na mafundisho ya mambo mbali mbali. Mwangaza news ni blog inayokupa vitu uvipendavyo ambavyo hutapata kwenye blog nyingine Tanzania.
Tembelea blog hii kila siku ufaidike na upate maarifa mbali mbali toka mwangaza news. Unaweza kutoa maoni yako hapa chini. Pia share blog hii facebook twitter yahoo instagram whatsapp na kwingineko ili watu wengi waje kupata mwanza news

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)