Jumanne, 23 Mei 2017

UN WAIOMBA PYONGYANG KUSITISHA HARAKATI ZAKE ZA KUENDELEA NA MAJARIBIO YA KURUSHA MAKOMBORA

Tags

Umoja wa Mataifa umeiomba Korea ya Kaskazini "kusitisha mara moja majaribio yake ya Makombora ya masafa marefu ambayo yanahatarisha Usalama wa Kimataifa''.


Kuendelea kwa Korea ya Kaskazini na majaribio yake ya kurusha Makombora ya masafa marefu,"kuna maanisha kwamba Korea ya Kaskazini inapinga Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."



Raia wa Korea ya Kaskazini wakiangalia kupitia televisheni habari kuhusu urushwaji wa Kombora Mei 22,2017 pic.AFP



Korea ya Kaskazini imesema Siku ya Jumatatu Mei 22,2017  kuwa ilifaulu kurusha Kombora la masafa marefu ya wastani licha ya kukabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapiga marufuku kujihusisha na kufanya majaribio ya Makombora ya masafa marefu.

Washington pia inafanya mazungumzo na Beijing,mshirika mkuu wa Pyongyang, kuhusu Azimio jipya la kuongeza shinikizo  kwa Serikali ya Kikomunisti ya Pyongyang.


EmoticonEmoticon